Kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania cha Pool Table kimeendelea na mazoezi katika club ya Sniper Mwenge Mpakani kujiandaa na michuano ya Afrika itakayofanyika nchini Afrika kusini Oktoba 11 hadi 16 mwaka huu.
Wachezaji hao chini ya kocha mkuu Denis Lungu wanafanya mazoezi kila siku kuanzia saa sita mchana hadi saa moja na nusu usiku ili kujiweka fit na maandalizi ya mchezo huo.
Kikosi hicho ambacho kinawachezaji tisa wanaume na sita wanawake lengo lake kubwa ni kutafuta wachezaji saba wakiume watakao ungana na Omary Akida ambaye anacheza pool ya kulipwa nchini Afrika kusini kutengeneza timu ya waacheaji nane watakao wakilisha kwa` upande na wa wanaume na kwa upande wakina mama wachezaji wote sita watasafiri kuwakiliisha nchi nchini Afrika Kusini.
Ili kuendelea kukuza mchezo wa pool table nchini Chama cha Pool Table Tanzania (TAPA) kimedhamiria kupeleka mchezo katika mikoa yote ya Tanzania kwa kufanya mashindano maalum Monthly Mug) yatakayokuwa yakifanyika kila baada ya miezi mitatu.
Mwenyekiti wa TAPA Willfred Makamba amesema lengo la kuanzishwa kwa mashindano hayo ni ili kutoa nafasi kwa Mikoa mbali mbali pamoja na wachezaji wao kupata fursa ya kushiriki katika mashindano hayo.
Kwa upande wa wachezaji wameonesha kufurahishwa na kuanzisha kwa `mashindano hayo kwasababu yatakuwa ni daraja zuri kufikia malengo yao kwa kuonesha vipaji walivyonavyo.